PATANISHO:Mume wangu aliniambia kuwa wanashare mimba yangu

Muhtasari

 • Patanisho

 • Mume wangu wanashare mimba

 • Hatukuwa na amani nyumbani kwao

 •Tumekuwa tukizozana 

Gidi na Ghost
Image: Radiojambo

Leo katika kipindi chapatanisho Bi Audrey alituma ujumbe ili apatanishwe na mumewe Kiprop ambaye alimwambia kwamba 'wanashare'  mimba na mwanamume mwingine.

"Nimekuwa nikikosana na mume wangu kwa muda naenda kwetu kisha ananirudisha, kwao sikuwa na amani kwa maana watu wa kwao walinitenga kwa sababu mimi si mnandi kama wao".

"Tulihama kwao tukaenda kuishi Kitale, hivi juzi alinirudisha baada ya kwenda kwetu, nilipata mimba baada ya yeye kushinda kunifuata. Wiki jana nilipokuwa hospitalini alinitumia ujumbe akiniambia kuwa wanashare mimba yangu na mwanamume mwingine ambaye aliposti kwenye facebook".

"...mimi nampenda na nataka nijue kwanini alisema hayo, kwa maana baada ya kuniambia maneno hayo alibadilika kabisa hata haniongeleshi wala kushughulikia ujauzito wangu," Alieleza Audrey.

Baada ya muda mfupi bwana Kiprop alipopigiwa simu alikuwa na haya ya kusema kuhusu madai ya mkewe.

"Mimi mambo hayo tulimaliza na nilisema hayo kwa hasira, ninakubali kuwa mimba ni yangu na wala si ya mtu mwingine, lakini nataka mke wangu aniheshimu."

(Mhariri  Davis Ojiambo)