Walienda wapi?Wanasiasa wakosa kuhudhuria mazishi ya vijana waliaga baada ya vurugu vya Murang'a

Muhtasari
  • Vijana hao waliaga dunia baada ya vurugu kuzuka eneo la Kenol
  • Wabunge na wanasiasa walidinda kuhudhuria mazishi hayo
  • Kung'u alikashifu kitendo hicho vikali sana
Mutyambai 2
Mutyambai 2

Vijana wawili waliopoteza maisha  yao katika eneo la Kenol wakati vurugu zilizuka kutokana na ziara ya Naibu Rais William Ruto walizikwa Ijumaa, Oktoba 16.

Ni vurugu na ghasia ambazo zilishtumiwa sana na viogozi huku kidole cha lawama kikinyoshewa naibu rais William Ruto.

Baada ya hayo  wanasiasa wengi hawakuhudhuria mazishi ya vijana hao yaliyofanyika Ijumaa,16 ina maana wanasiasa wanawatumia tu vijana kuzua vurugu na kisha mabaya yakitokea wanakwepa na kunyamza?

 

Wawili hao walifanyiwa ibada ya mazishi ya pamoja kabla ya kila familia kuchukua mpendwa wao kwa mazishi ya kifamilia.

Licha ya kuwa wawili hao walipoteza maisha yao kutokana na ghasia zilizozinduliwa na makundi ya Kieleweke na Tangatanga yaliyochochewa na viongozi, hakuna mwanasiasa hata mmoja wa pande hizo alihudhuria ibada hiyo.

Hata hivyo ni wanasiasa James Nyoro, gavana wa Kiambu, na William Kabogo ndio waliohudhuria mazishi hayo.

Viongozi waliwataka vijana kujiepusha na wanasiasa ambao wanawatumia kwa maslahi yao binafsi na kisha kuwatelekeza.

Aidha kapteni Kung'u Muigai alikashifu kundi la wanasiasa kutokana na vifo vya wawili hao.

"Kama wewe ni mwanasiasa ambaye anasababisha mambo kama haya kutokea hatuwezi kujihusisha na wewe. Hata uwe nani ama nani." Alisema Kung'u.

Mbunge Nyoro na mwenzake Wahome walikuwa wametakiwa kurekodi taarifa kuhusiana na ghasia hizo lakini wakadinda.

Kutoka kwetu wanajambo MUngu alaze roho zao mahali pema peponi.