Reggae ya BBI imerudi: Raila asema haya baada ya kupokea ripoti ya BBI

Muhtasari
  • Ripoti ya BBI kusomwa mnamo tarehe 26, Oktoba 2020 katika eneo la Bomas
  • Mazungumzo ya BBI si ya kumfanya Raila rais wala Uhuru waziri mkuu

Baada ya rais Uhuru Kenyatta na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kupokea ripoti ya BBI walizungumza mambo kadha wa kadha huku kinara Odinga akikashifu sana mradi wa naibu rais William Ruto huku  akisema kuwa saa hizi ndio amekumbuka kuwa wakenya wanahitaji mkokoteni.

"Unaweza aje shugulikia maswala ya wakenya kama huwafahamu vyema, wengi watasema ya kwamba wametambua kuwa wao ni wakenya wakiwa kwenye umaskini wao na unataka kuzungumza na wakenya maskini

Mawasiliano na mazungumzo haya yameanza, hii si kumfanya Raila awe kiongozi wala Uhuru Kenyatta awe waziri mkuu haya ni mapendekezo hayajatupwa kwa mawe tutakusanya saini na tuzipeleke IEBC na natumai bunge litakamilisha kwa wiki moja." Alisema Raila.

Huku Rais akizungumza ni lini BBI itasomwa na kueleza wananchi pointi moja kwa moja alikuwa na haya ya kusema.

"Tutaonana kule Bomas, kwa sasa, tunashukuru wenzetu wa Kisii kwa kutukaribisha. Sasa tutaingia pale town... Baada ya hapo tuwasalimie ndugu zenu wa Nyamira... Na mwishowe Raila atanionyesha hiyo fishing amesema kule Kisumu, kama hujaonja huwezi kujua." Uhuru Aliongea.

Vigogo hao wawili walipokea ripoti hiyo walipokuwa katika ikulu ndogo ya Kisii.