Kinara wa ODM Raila Odinga awashtumu wanaopinga BBI

raila odinga na Ruto
raila odinga na Ruto

Kiongozi wa ODM Raila Odinga amewashtumu wale wanaopinga BBI akisema kuwa ripoti hiyo haikusudiwa kuhakikisha kuwa anakuwa Rais au Waziri Mkuu bali ni kuunda amani na umoja nchini kwa vizazi vijavyo.

Amepuuzilia mbali madai kwamba BBI itaongeza mswada wa mapato wa nchi hiyo akisema kwamba waziri mkuu na manaibu wake watachaguliwa kutoka kwa wabunge na hivyo hakutakua na  mzigo wowote kwa mlipa ushuru.

Hata hivyo, mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amemkashifu kiongozi wa ODM Raila Odinga na watetezi wengine wa BBI kwa kushutumu IEBC kama sehemu ya shida katika kila uchaguzi.

Chebukati anasema Raila na wenzake wanatumia tume hiyo kwa njia isiyo ya haki. Anasema  ripoti ya BBI inapunguza tena faida iliyopatikana kwa miaka mingi kuhusu  usimamizi wa uchaguzi nchini.