Sonko anaamini kuwa nammaliza kisiasa sina tamaa ya siasa-Generali Badi

Muhtasari
  • Sonko anapaswa kuchukua faida ya kazi ya NMS na kupiga kampeni nayo mwaka wa 2022
  • Kusimamia mji ni kama kusimamia jeshi, Mohamed Badi asema
  • Anaamini kuwa nammaliza kisiasa

Ni vita ambavyo vimeshuhudiwa kati ya gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko na Mkuu wa NMS Mohamed Badi, hii ni baada ya rais Uhuru kumpa Badi majukumu ya kaunti ya Nairobu.

Badi akiwa kwenye mahojiano na runinga moja humu nchini, alimwambia gavana huyo hawache kumpiga vita badala yake asifu kazi ambayo NMS imefanya katika kaunti ya Nairobi.

Generali huyo alisema kuwa hajaweza kuelewa kwanini gavana huyo anampiga vita huku atupilia mbali madai kuwa alikuwa anammaliza kisiasa na kusema kuwa hana maazimio wala tamaa ya siasa kama alivyosema awali.

"Anaamini kuwa nammaliza kisiasa na wala sina maazimio ya kuwa mwanasiasa wala tamaa ya siasa

Nilisema hayo awali na mimemwambia hayo mara kadha wa kadha, ukweli ni kuwa anapaswa kuchukua faida kwa yale nimetenda na kunipongeza lakini hafanyi hayo anachagua kunipiga vita." Badi alisema.

Major General Mohamed Abdalla Badi
Major General Mohamed Abdalla Badi

Badi alisema kwamba alichagua kujibu vita hivyo kwa kimya ili gavana huyo asitambue alichokuwa anafanya.

"Sifurahishi matusi yeyote wala mashataka aliokuwa anasema kila wiki, siku moja ananiita ndugu wiki ifuatayo nastahili kuenda ICC

Usiku huo nilienda moja kwa moja hadi soko la Muthurwa kusimamia lori za NYS ili ziweze kubeba takataka."

Generali huyo alisema ya kwamba hakuweza kutekeleza mipango yake mipya bali alizingatia mipango ambayo aliipata kwenye ratiba.

Aidha alisema kuwa kusimamia mji ni kama kusimami jeshi.