Video ya muuguzi akichukua selfie na mjamzito katika maumivu ya leba yavutia hisia mseto

Wengine walimtetea nesi huyo wakidai huenda ni familia ya mwanamke huyo au hata yeye mwenyewe alimtaka kurekodi matukio ya kabla ya kujifungua kwa faida yake baada ya kuenda nyumbani.

Muhtasari

• Licha ya masikini huyo kulia kwa uchungu, muuguzi huyo hata hivyo aliendelea kufanya video ya mwanamke huyo mjamzito na kutabasamu.

Nesi akijirekodi kwenye wadi ya leba
Nesi akijirekodi kwenye wadi ya leba
Image: Screengrab

Video ya kutatanisha ya muuguzi wa kike akipuuza majukumu yake kwa mtindo wa maisha ya mitandao ya kijamii imekuwa ikienea mtandaoni na kwa kuongeza, ilizua gumzo pevu.

Mama mjamzito, anayeonekana kukaribia kujifungua, alionekana akiwa hana raha kwenye kitanda cha hospitali, lakini nesi, aliyeketi kando yake, aliamua kutumia tukio hilo la kusikitisha kuunda maudhui ya kujifaidi mitandaoni badala ya kumsaidia.

Katika klipu hiyo iliyosambazwa mtandaoni, muuguzi huyo, akiwa amevalia sare ya majukumu yake ya kijani kibichi, alionekana akipiga video ya selfie na mwanamke mjamzito katika leba.

Licha ya masikini huyo kulia kwa uchungu, muuguzi huyo hata hivyo aliendelea kufanya video ya mwanamke huyo mjamzito na kutabasamu.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii, waliotazama video hiyo, walionyesha hasira zao kwa muuguzi huyo, ambaye alichagua kuacha majukumu yake ili kuunda maudhui.

Wengine walimtetea nesi huyo wakidai huenda ni familia ya mwanamke huyo au hata yeye mwenyewe alimtaka kurekodi matukio ya kabla ya kujifungua kwa faida yake baada ya kuenda nyumbani.

Tazama video hiyo hapa chini kisha utoe maoni yako;