Nifungeni jela kuna maisha huko, kunamaisha baada ya siasa-Mike Sonko asema

Muhtasari
  • Sonko alisema kwamba hataachili pesa zozote mpaka pale NMS itahalalishwa
  • Gavana huyo aloisema kwamba afungwe lakini kuna maisha baada ya kufungwa na kifo
mike sonko
mike sonko

Gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter amesema kwamba hatakubali vitisho vya wapinzani wa kisiasa.

Pia Sonko alisema kwamba yuko karibu kukufa kwa ajili ya kushikilia katiba ya kenya kwa kufanya kazi ambayo inastahili katika sekta yake.

Pia alisema kwamba hataachilia fedha ili kumpa bosi wA NMS kwa maana ni kinyume cha sheria na katiba.

 

" Nina suluhisho za kupendeza lakini nini haswa hutendeka tunapokutana katia mkutano ili kutoa suluhisho hizi ndiposa wakazi wa Nairobi wapate huduma nzuri huwa tunatofautiana katika sheria kina chofuata ni vitisho

Siku za gia zimepita sitamkubali mtu kunitishia kwa ajili ya sheria, wacha tufuate sheria na kisha wahalalishe NMS nitaachilia pesa." Sonko aliongea.

Sonko alikuwa mbele ya kamati ya seneti ili kujibu maswali kuhusu kuachilia kwa fedha hizo.

"Nifungeni jela, kuna maisha baada ya siasa, niueni lakini bado kuna maisha baada ya kifo ambapo mwendazake baba yangu, mababu wa nchi yetu kama mzee Jomo Kenyatta wamelala kwa amani lakini hakuna kiasi cha vitisho." Sonko Alizungumza.