Kalonzo,Mudavadi,Wetangula wakubaliana kufanya kazi pamoja huku siku za uchaguzi zikiwadia

Muhtasari
  • Kalonzo,Mudavadi,Wetangula wakubaliana kufanya kazi pamoja huku siku za uchaguzi zikiwadia
  • Viongozi hao walishauriwa na Charity Ngilu wafanye kazi pamoja na kushikana mkono

Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, kiongozi wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi na wa chama cha Ford Kenya Moses Wetangula wamekubaliana kufnya kazi pamoja huku miezi chache ikisalia mbele ya uchaguzi mkuu.

Vingozi hao ambao waliungana na gavana wa kaunti ya Kitui Charity Ngilu, walikuwa na mkutano huo siku ya Jumanne ambapo walijadiliana mambo kadha wa kadha.

Viongozi hao walisema kwamba hawapingi ripoti ya BBI bali wanaunga mkono ripoti hiyo ilhali inahitaji marekebisho.

Kwa upande wake Wetangula alikuwa na haya ya kusema;

"Tutatembea pamoja hii sio uvumbuzi, tumefanya hivyo hapo awali; si mara moja, si mara mbili." Wetangula alisema.

Ngilu aliwahimiza vigogo hao washikane mkono na kutembea pamoja kwa maana wakitengana hawawezi enda na mbele.

Mudavadi naye aliwashauri wakenya wamalizane na BBI kwa maana imekawia sana.

"Kuna kitu nataka kuwauliza Wakenya, tunahitaji kutoa mjadala huu wa BBI, tumalizane nayo,kwa miaka miwili na nusu tumekuwa tukizungumzia BBI 

Hatupaswi kuingia mwaka wa 2022 tukizungumzia BBI bado."

Naye kinara wa Wiper alikuwa na haya;

"Kwa kuepusha shaka, kikundi hiki kinasaidia kikamilifu ripoti ya BBI, hiyo ni wazi kabisa, kwa kweli Mudavadi alikuwa ananiambia kuwa ni jambo ambalo limekamilika 

Lakini ambacho tunataka kuwaambia wakenya kuwa kilicho mbele yao ni rasimu ya muswada

IEBC ikimaliza kukagua saini watapeana rasimu ya mwisho." Kalonzo Alizungumza.