William Ruto aliwachochea wakazi wa mlima kenya dhidi ya uhuru Kenyatta-Mutahi Ngunyi

Muhtasari
  • Mutahi Ngunyi adai kwamba William Ruto aliwachochea wakazi wa mlima kenya dhidi ya rais Uhuru Kenyatta
  • Pia mchanganuzi huyo alisema kwamba njia bora ya kumuangamiza Ruto ni kumnyang'anya wakikuyu
zjCk9kqTURBXy8yM2RiNzY4ZTY4MjAzMzg2Zjc5YTgzMjAxMTg4YWQ5MC5qcGVnkZMFzQMUzQG8gaEwAQ
zjCk9kqTURBXy8yM2RiNzY4ZTY4MjAzMzg2Zjc5YTgzMjAxMTg4YWQ5MC5qcGVnkZMFzQMUzQG8gaEwAQ

Mchanganuzi wa siasa Mutahi Ngunyi amekaangwa mtandaoni baada ya kuchochea siasa za kikabila kwenye ulingo wa kisiasa.

Mutahi ambaye kwa kawaida ana mazoea ya kueneza siasa za kikabila kwenye mitandao ya kijamii alijipata pabaya baada ya kusema kwamba Ruto hawezi bila jamii ya mlima kenya na kuwa ndiye aliwachcochea wakazi wa mlima kenya dhidi ya rais.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Ngunyi alisema endapo Wakikuyu watatenganishwa na Ruto, atamalizwa kisiasa kwani Naibu Rais hawezi kutimiza azma yake bila Wakikuyu.

"Njia bora ya kumuangamiza William Ruto ni kumnyanganya Wakikuyu. Ni rahisi hivyo. Bila Wakikuyu, hakuna Ruto. Rafiki yetu anatembelea matope.Mvua ukimwagika kutoka GEMA utamfanya kukwama," aliandika Ngunyi Jumatatu, Januari 4."

Wakenya walimsuta vikali kwa matamshi yake huku wengi wakimkubusha kuwa tayari Kenya imesonga mbele kutoka kwa siasa za kikabila.

Baada ya kusutwa vikali Ngunyi hakutia kikomo bali alisema kwamba ugomvi uliopo kati ya wakazi wa mlima kenya na Uhuru Kenyatta ulianzishwa na kuzalishwa na naibu wake William Ruto.

"William Ruto aliwachochea wakikuyu dhodi ya rais Uhuru Kenyatta, uasi wa GEMA  na uchochezi wa kikuyu dhidi ya UHuru Kenyatta zote zilizalishwa na Ruto kwa utaratibu

Lakini huu hapa ukweli aidha Ruto anawachezea wakikuyu au wakikuyu wanamchezea William Ruto kwa maana mimi ni mkikuyu." Mutahi Aliandika.

PIa Mchanganuzi huyo alisema kwamba wakikuyu watatoka madarakani kwa miaka 30 ijayo, na kuwa maisha yao ya usoni inapaswa kuamulikwa kwa siku 365 na kuwa William Ruto si maisha yajayo ya jamii ya kikuyu.