Nilipewa milioni 17 kumsaliti Mudavadi-Mbunge Savula adai

Muhtasari
  • Mbunge Savula afichua siri kuhusu Mudavadi huku akiwahotubia waombolezaji
  • Mbunge huyo alifichua kuwa Mudavadi alimlipia karo ya shule
Kinara wa ANC Musalia Mudavadi. Picha:HISANI
Kinara wa ANC Musalia Mudavadi. Picha:HISANI

Mbunge wa Lugari Ayub Savula akihotubiwa waombolezaji katika ibada ya wafu ya Mama Hannah Mudavadi, alifichua kwamba kuna mtu ambaye alikuwa amempa milioni 17 ili kumsaliti kinara wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi.

Savula alisema wakati chama hicho kilikuwa kinakabiliana na shida tofauti mwaka wa 2020,na wanachama kupanga kumtimua Mudavadi kama kiongozi wao ndio wakati alikuwa anaambiwa achukue milioni hizo.

Ni wakati ambao mbunge huyo alikuwa anaomboleza na kupanga mazishi ya baba yake Juni 2020.

 

"Nilipokuwa namzika baba yangu, mtu alikuja na helikopta hadi nyumbani kwangu na milioni 17, huku akiniambia niende nikamtoa mudavadi kama kiongozi wangu wa chama cha Amani National Congress

Nilikataa, na nikamwambia mimi ni mtoto wa muhubiri na ni familia ambayo ilinilea." Alidai Savula.

Huku akiendelea na kuzungumza pia alifichua kuwa familia ya kinara huyo ni kama yake na kwamba Mudavadi alimpeleka shule.

"Ninashukuru familia ya mwendazake Moses Mudamba Mudavadi kupitia kwake Musalia Mudavadi alinilipia karo ya shule hata nilipokuwa katika chuo kikuu alinilipia karo ya shule

Pia alimlipia mheshimiwa Osotsi karo ya shule na huo ndio ukweli."