'UJa uzito sio virusi,'CS Magoha asema wanafunzi walio na ujauzito wasakwe

Muhtasari
  • Waziri wa elimu George Magoha asema wanafunzi ambao hawajarejea shuleni kwa ajili ya ujauzito wanapaswa kusakwa na kurejeshwa shuleni
  • Pia alisema kwamba wizara inafuraha kwa ajili asilimia 80 ya wanafunzi wamerejea shuleni
  • Waziri huyo aliwaonya walimu wakuu dhidi ya kuwatumwa wanafunzi nyumbani kwa ajili ya karo ya shule
CS magoha
CS magoha

Uja uzito haupaswi kuchukuliwa kama virusi haya ni matamshi ya waziri wa elimu George Magoha aliotamka akiwa katika shule ya upili ya DEB katika kaunti ya Bungoma siku ya Ijumaa.

Magoha alisema kwamba ilikuwa lazima watoto wote warudi shuleni baada ya kuwa nyumbani kwa miezi kumi.

Pia waziri huyo aliagiza wanafunzi ambao hawajarejea shuleni kwa ajili ya ujauzito wasakwe na kisha wapewe ushauri ili waweze kurudi shuleni na kuendelea na masomo yao.

 

"Uja uzito haupaswi kuchukuliwa kama virusi, tunawahitaji maafisa wa wizara wa ndani wawasake wanafunzi ambao wanaujauzito na hawajaweza kurejea shuleni wapewe mawaidha kisha warudi shuleni

Tunashukuru shule ambazo zinahakikisha ya kwamba wanafunzi wanaendelea na kupokea masomo wakati huu." Aliongea Magoha.

Waziri alisema kwamba wizara hiyo ina furaha tele baada ya asilimia 80 ya wanafunzi kurejea shuleni

Magoha alisema kuwa serikali imetoa madawati yakutosha ili kuhakikisha wanafunzi wamesoma bila tashwishwi yeyote.

Pia alionya walimu wakuu wa shule dhidi ya kuwatuma wanafunzi nyumbani kwa ajili ya karo ya shule, huku akiwaamia wanapaswa kuelewa jinsi uchumi umekuwa mbaya kwa ajili ya janga la corona.

Shule zilifungwa rasmi mwezi wa machi 2020 baada ya kisa cha kwanza cha virusi vya corona kuripotiwa nchini.

"Kwa shule za msingi na sekondari hatupaswi kuwa na mjadala kwa ajili ya karo,kwa maana serikali tayari imetoa pesa kwa mashule, hakuna mwanafunzi anapaswa kurudishwa nyumbani."