Covid-19: Wawili waaga dunia huku Kenya ikirekodi visa 223 vipya

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe

Siku ya Jumamosi Kenya ilirekodi visa 223 vipya vya Covid-19 kutokana na sampuli 7,748 zilizopimwa.

Hii inafikisha idadi ya visa vilivyoripotiwa kufikia 99,082, waziri wa afya Mutahi Kagwe asema..

Kupitia taarifa, waziri Kagwe alithibitisha kuwa vipimo vilivyofanywa vimefikia 1,121,946 kufikia sasa.

Visa vya watu walioaga dunia vimeongezeka na kufikia 1,728 baada ya wagonjwa wawiliwaliougua Covid-19  kuaga dunia.

Hata hivyo wagonjwa 129 wamepona kutokana na ugonjwa huo.

Idadi ya waliopona sasa imedikia 83,324.