Sonko alisema ulikuwa mpango wenu-Octopizzo ampa Dennis Itumbi vijembe baada ya kusema vijana wa Kibra ni wezi

Muhtasari
  • Octopizzo amshambulia Dennis Itumbi baada ya kusema vijana wa kibra ni wezi ambao wanatumiwa na wanasiasa
octopizzo
octopizzo

Rappa Octopizzo amemshambulia Dennis Itumbi baada ya kusema kwamba vjana wa mtaa wa Kibra wanatumiwa na wanasiasa kucchoma mikokoteni ya 'Hustler nation'.

Pia Octopizzo aliwaambia wanasiasa na viongozi wengine wawache kuwatumia vijana kuvuruga mikutano ya kisiasa kwa ajili ya mafanikio yao wenyewe.

Cheche za maeneno zilishuhudiwa kwenye miyandao ya kijamii ya twitter, huku rappa huyo akimwambia Itumbi kwamba Sonko ashaafichua siri kwamba kuhusu mapigano ya mwaka wa 2017.

 
itumbi
Dennis Itumbi itumbi

"Wezi wanasafirishwa kutoka kibra kuchoma wheelbarrows na mikokoteni, Gihurai, wanafuata maagizo kwamba hawataki mikokoteni bali wanataka BBI." Aliandika Itumbi.

Kwa haraka Octopizzo alikuwa na haya ya kusema kuhusu usemi wake Itumbi,

"Sonko alisema ulikuwa mpango wenu kisha mkaekelea chama cha upinzani,@OleItumbi acha ujinga.

Kwa heshima tuambie deep state ni akina nani? kwa maana tunajua nchi hii imesimamiwa na rais na naibu wake ambayo huwa tunaita ikulu tambulisha mmoja wao So tuchanue mtuangu @OleItumbi." Octopizzo alijibu.

Pia kupitia kwa ujumbe mwingine Octopizzo alisema kwamba vijana wa Kibra wamekuwa na maisha magumu kwa ajili ya wanasiasa.

"Vijana wa kibra wanalaumiwa kila wakati, wanatumika na kisha kuitwa wezi, wakati wote wa jambo lolote la kisiasa

Hii imewafanya vijana ambao si wezi kutopata kazi nchini kwa ajili ya kauli ya wanasiasa na mambo hayo, huu ujinga unapaswa kusimamishwa."

 

Octopizzo alisema kwamba kuna baadhi ya vjana ambao wamehitimu kuliko hata wanasiasa wenginw serikalini.