Watu 200,000 wanahitaji msaada Mandera

Gavana wa Mandera Ali Roba

Takriban  watu 200,000 huko Mandera wanahitaji msaada wa chakula. Gavana Ali Roba anasema kuwa hii ni asilimia 30% ya idadi ya kaunti na anaonya kuwa ikiwa serikali na wafadhili watakosa kuingilia kati  kuokoa hali hiyo, kaunti pekee haitaweza kudhibiti hali hiyo.

Hayo yakijiri, jamii  zinazoishi katika kaunti ya  Garissa zimeagizwa kuishi kwa amani na kumaliza mapigano ya mara kwa mara kati yao.

Baraza la Wazee la Garre linalo ongozwa na Ali Noor Ibrahim linasema maendeleo yanaweza kupatikana tu pale kunapokuwa na amani.

Kwingineko, jumla ya watu 12,000 wamechanjwa  katika kaunti ya Bungoma kufikia sasa. 8,000 ya idadi hiyo walichanjwa wiki iliyopita pekee huku watu wengi wakiendelea kujitokeza kupata chanjo hiyo. Kaunti hiyo  ilipokea dozi 22,000 za chanjo ya AstraZeneca. 

Wakazi wa Kimilili huko Bungoma wanaishi kwa hofu kufuatia visa vingi vya mashambulio ya genge la wahalifu katika eneo hilo. Wakazi hao wanasema watu kadhaa wameuawa na wafanyibiashara kuibiwa na majambazi wenye silaha wakati wa saa za kafyu.

Juzi usiku genge hilo lilimuua mlinzi katika mji wa Kimilili .