Barabara jijini Nairobi kufungwa kutokana na ukarabati unaoendelea

barabara ya bunyala kufungwa
barabara ya bunyala kufungwa

Barabara ya Bunyala na mzunguko wa uwanja wa Nyayo kwa siku ya tatu imefungwa kwa trafiki ili kutengeneza njia kwa  ujenzi wa  Nairobi Express way.

KENHA inasema sehemu hiyo itabaki imefungwa kwa siku 20 hadi Aprili 29 na wenye magari kwa hivyo wanapaswa kutafuta njia mbadala kutoka CBD wakitumia Barabara ya Bunyala, Barabara ya Lusaka au barabara ya Aerodrome.

Hayo yakijiri, ambulensi ya Kenya Redcross  jana usiku lilihusika katika ajali eneo la  Ratabei huko Kabarnet, Kaunti ya Baringo wakati ilipokua ikimpeleka  mgonjwa kwenda hospitali ya Kabarnet kwa rufaa.

Inadaiwa kuwa ambulensi hiyo ilikuwa likiendeshwa na dereva mlevi. Mgonjwa huyo alijeruhiwa na kupelekwa hospitali ya Kabarnet kwa matibabu.

Chama cha mawakili LSK kimeuliza serikali kurudisha misaada ya ushuru iliyowekwa mwaka jana ili kuwalinda Wakenya na wafanyabiashara kutokana na athari za kufungwa kwa kaunti 5. Mkurugenzi Mtendaji Mercy Wambua anasema mamilioni ya watu wamepoteza mapato kwa kupoteza kazi na kupunguzwa mishahara tangu  amri ya curfew ya 8 usiku kutolewa.

LSK inaonya kuhusu  kuongezeka kwa uhalifu ikiwa serikali haitaingilia kati na kusaidia wananchi. 

Tume ya huduma ya mahakama  JSC kuanzia kesho itaanza kukagua wagombea kumi walioteuliwa kuhojiwa kwa nafasi ya Jaji Mkuu kuchukua nafasi ya David Maraga aliyestaafu.

Jaji Said Chitembwe atakuwa wa kwanza kukabiliana na jopo hilo kesho akifuatiwa na Profesa Patricia Mbote Jumanne wakati Ijumaa tarehe 23 mwezi huu itakuwa siku ya mwisho ya mahojiano na Alice Jepkoech akifunga ukurasa wa mahojiano hayo kama mgombea wa kumi na wa mwisho.

 Wamiliki wa biashara katika mji wa Eldoret wameulizwa kutekeleza kwa ukali itifaki zote za Covid-19 ndani ya majengo yao na kusaidia kuzuia kuenea kwa virusi ambavyo sasa vinazidi kusambaa.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Uasin Gishu Willy Kenei amewashauri wamiliki wa baa, hoteli na maduka ya jumla kutekeleza kanuni kwa makini  kwani wataathirika zaidi iwapo kaunti hiyo itafungwa.