Covid-19:Watu 1,091 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Kenya imerekodi visa 1,091 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 5,958 katika muda wa saa 24 zilizopita
Eatw-C2X0AAX1vP.jfif
Eatw-C2X0AAX1vP.jfif

Kenya imerekodi visa 1,091 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 5,958 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 149,219 kutoka kwa sampuli 1,584,731.

Katika visa hivi vipya, 1,060ni raia wa Kenya huku 31 wakiwa raia wa kigeni, 619 ni wa kiume na 472 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana mwaka 1 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 98.

Jumla ya wagonjwa 1,603 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 5,567wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 261 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)