'Ulinifunza mengi!' Ghost Mulee amsifia mamake miaka 25 baada ya kifo chake

Kila mmoja anahitaji upendo wa mama mzazi na haijalishi umri wako au hadhi yako ya kijamii, kwani upendo huo ni wa kipekee na usiopatikana kokote kule.

Mtangazi wa Rado Jambo, Ghost Mulee anafahamu hili zaidi kwani ni upendo ambao hajaweza kuupata tena kwa miaka 25, tangia mamake mzazi, Maria Wanza Musyoki kuaga dunia.

Ghost alichapisha picha ya mamake ambaye alikuwa na urembo wa kupindukia huku akimsifia kwa yale aliyomfanyia akiwa uhai.

"Mamangu Maria Wanza Musyoki endelea kupumzika kwa amani!! Ulinifunza mambo chungu nzima. Imepita miaka 25 sasa!" Aliandika Ghost.

Mtangazaji huyo hajakuwa hewani kwa mda sasa kwani alisafiri hadi India kwenda kupokea matibabu.

Hapo jana, alichapisha picha akiwa hospitalini pamoja na nduguye na daktari huku akidai kuwa anashukuru kuwa mambo yanaendelea vyema na anaendelea kupata nafuu.

Tazama picha zifuatazo;

Ni furaha yetu sote kuwa 'coaches' anaendelea kupata nafuu na tunamuombea uponyaji wa haraka ili aweze kurejea kazini.