Covid-19:Watu 568 wapatikana na corona,173 wapona huku 15 wakiaga dunia

Muhtasari
  • Kenya siku ya IJumaa ilirekodi visa 568 vya maambukizi ya corona kutokana na sampuli 9,029 zilizopimwa chini ya saa 24
  • Asilmia ya maambukizi nchini kwa sasa imefika 6.3%

Kenya siku ya IJumaa ilirekodi visa 568 vya maambukizi ya corona kutokana na sampuli 9,029 zilizopimwa chini ya saa 24.

Idadi jumla ya watu waliopatikana na corona imefika 162,666, huku jumla ya sampuli zilizopimwa zikifika 1,710,414.

Kati ya maambukizi hayo mapya 551 ni raia wa kenya ilhali 17 ni raia wa kigeni,344 ni wanaume huku 224 wakiwa wanawake.

 

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana mwaka mmoja huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 105.

Asilmia ya maambukizi nchini kwa sasa imefika 6.3%.

Kulingana na wizara ya afya watu 173 wamepona maradhi hayo na kufikisha idadi jumla ya 110,653, Watu 130 walipona wakiwa wanapokea matibabu nyumbani huku 43 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Vile vile, kwa habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 15 wameaga dunia kutokaana na corona na kufikisha idadi jumla ya 2,865 ya watu walioaga kutokana na corona.

Kuna Wagonjwa 1,086 waliolazwa hospitalini nchini huku 6,381 wakipokea matibabu wakiwa wamejitenga nyumbani.

Huku hayo yakijiri wagonjwa 131 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi nchini.

Kufikia siku ya ijumaa idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 911,515.