Fainali ya kombe la ligi ya mabingwa itachezwa nchini Ureno

kombe la ligi ya mabingwa
kombe la ligi ya mabingwa

Fainali ya kombe la Champions League ya Chelsea dhidi ya Manchester City itachezwa nchini Ureno katika uwanja wa Estadio do Dragao huku mashabiki elfu 6 kutoka kila pande wakiruhusiwa kutazama.

Hapo awali mechi hiyo ilipangiwa kuchezwa Istnabul Uturuki, ila nchi hiyo ni miongoni mwa nchi zilizopigwa marufuku kusafiri na serikali ya Uingereza kutokana na janga la corona.

Tukirejea nchini, shirikisho la riadha nchni limethibitisha kuwa mbio za majaribio ya Olimpiki zitakua za mwaliko na wala sio za wanaridha.

Huku zikiwa zimesalia chini ya miezi miatu michezo ya Tokyo Japan kuanza, Afisa wa AK Paul Mutwii anadai hawana muda wa kuwajaribu wanariadha wote. Wakimbiaji walifikisha muda wa kufuzu katika mbio za Diamond League na za dunia na wataalikwa kupigania nafasi za michezo ya Tokyo.