Mwendeshaji wa bodaboda auliwa na stima Bungoma

Alikuwa akiosha pikipiki yake kwenye kidimbwi kidogo cha maji kando ya barabara bila kujua kuwa kuna waya ya stima iliyokuwa imeanguka hapo

Muhtasari

•Alikuwa akiosha pikipiki yake kwenye kidimbwi kidogo cha maji  kando ya barabara bila kujua kuwa kuna waya ya stima  iliyokuwa imeanguka hapo

•Wakenya wamesuta kampuni ya KPLC kwa kutokuwa  makini kazini

kplc
kplc
Image: file

Kijana mmoja mwendeshaji wa bodaboda upande wa  Kanduyi  aliuliwa na nguvu za umeme katika  kando ya barabara ya Kanduyi-Malaba mapema wiki hii.

Inadaiwa kuwa kijana huyo alikuwa ameenda kuosha pikipiki yake mahala ambapo palikuwa pamekusanyika maji ya mvua bila kujua kuwa kuna waya ya stima iliyokuwa kwenye maji hayo.

Kampuni ya umeme nchini Kenya(KPLC) imetangaza kuwa inatambua  kuhusu mkasa huo na inashirikiana na polisi katika kufanya uchunguzi .

Tunasikitishwa na tukio hilo na tumejitolea kabisa kuhakikisha kuwa suluhisho linapatikana” shirika la KPLC liliandika.

Baadhi ya Wakenya mtandaoni wamesuta kampuni ya KPLC kwa kukosa uwajibikaji na kutojali maslahi ya wanamchi. Pata hapa  baadhi ya hisia za Wakenya.

Mkaazi mmoja wa eneo hilo amearifu Radio Jambo kuwa huo sio mkasa wa kwanza wa aina hiyo kutokea upande huo.