Naomi Campbell ajaliwa mtoto wa kwanza akiwa 50

Balozi wa Magical Kenya ametangaza kuwa amepata mtoto kupitia mtandao wa Instagram

Muhtasari

•Campbell aliteuliwa kuwa balozi wa Magical Kenya mwezi wa Januari mwakani

•Ana umri wa miaka 50

Naomi Campbell
Naomi Campbell
Image: Hisani

Mwanamitindo na mcheza filamu Naomi Campbell tokea Uingereza, Naomi  Campbell ametangaza kupata mtoto wake wa kwanza.

Mwamitindo huyo ambayen awali mwakani aliteuliwa kuwa balozi wa kimataifa wa utalii nchini Kenya ametangaza ujio wa mtoto huyo siku ya Jumanne  akiwa na umri wa miaka 50.

Campbell aliyeonekana mwenye bashasha alitangaza kupitia ujumbe aliochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

“Kiumbe kirembo kimechanichagua mimi niwe mama yake, ni na raha sana kuwa naye na hakuna maneno yanayoweza kueleza uhusiano mwema ninao nawe malaika wangu. Hakuna mapenzi zaidi” Campbell aliandika chini ya picha ya kitoto alichoshika kwa mkono.

Hata hivyo, mwanamitindo huyo mzaliwa wa Jamaica hakutambulisha jina ama jinsia ya mtoto yule.

Kuteuliwa kwa Campbell kuwakilisha wizara ya utalii Kenya awali mwakani uliibua hisia mbalimbali baina ya Wakenya huku wengi wakionekana kusuta hatua hiyo. Wakenya wengi mtandaoni walimkashifu waziri Balala kwa kumpa mgeni nafasi ile.