Covid-19: 23 waaga, visa 166 vipya vyaripotiwa

Hii leo watu 166 wameambukizwa virusi vya Corona kutokana na sampuli 3,561 zilizopimwa.

Kutokana na visa hivyo, 156 ni wakenya huku 10 wakiwa wageni. 116 ni wanaume huku 50 wakiwa wagonjwa wa like.

Mgonjwa mchanga zaidi ana umri wa miaka minne huku mkongwe zaidi akiwa na miaka 97.

Kufikia sasa idadi ya visa vilivyoripotiwa humu nchini vimefikia 172, 491 huku idadi ya sampuli zilizopimwa zikifikia 1,834, 247.

Habari njema ni kuwa wagonjwa 93 wamepata nafuu. Katika habari za tanzia ni kuwa kumeripotiwa vifo 23 visa ambavyo sio vya masaa 24 yaliyopita ila ni visa vilivyotokea katika mwezi wa nne na wa tano.

Hii inaamisha kuwa kufikia sasa ni watu 3,287 walioaga kupitia virusi hivyo.

Wizara ya afya imeripoti kuwa kufikia sasa watu 8,181 wamepokea chanjo yao ya pili