Covid-19: Watu 488 wapatikana na corona,343 wapona,16 waaga dunia

Muhtasari
  • Watu 488 wapatikana na corona, 16 waaga dunia
  • Kati ya visa hivyo vipya 481  ni wakenya ilhali 7 ni raia wa kigeni,315 ni wagonjwa wa kiume huku 173 wakiwa wa kike.

Visa 488 vipya vya maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini siku ya JUmatano kutoka kwa sampuli 5,831 na kufkisha idadi jumla ya 174,773 vya maambukizi ya maradhi hayo.

Kati ya visa hivyo vipya 481  ni wakenya ilhali 7 ni raia wa kigeni,315 ni wagonjwa wa kiume huku 173 wakiwa wa kike.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 3 ilhali mwenye umri wa juu ana miaka 94.

Kulingana na wizara ya afya watu 343 wamepona maradhi hayo na kufikisha idadi jumla ya 119,589 ya watu waliopona corona.

274 wamepona wakipokea matibabu wakiwa nyumbani huku 69 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hopitali mbalimbali nchini.

Kwa habari za kuhuzunisha ni kuwa watu 16 wameaga dunia kutokana na corona na kufikisha idadi jumla ya 3,378 ya watu walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 969 ambao wamelazwa hospitalini, huku 4,827 wakipokea matibabu wakiwa nyumbani.

Vile vile wagonjwa 162 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).