Covid-19: watu 535 wapona corona,456 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Kenya siku ya jumanne imerekodi visa 456 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 5,626 katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 176,137 kutoka kwa sampuli 1,876,105
  • Katika visa hivi vipya, 424 ni raia wa Kenya huku 32 wakiwa raia wa kigeni, 266 ni wa kiume na 190 ni wanawake

Kenya siku ya jumanne imerekodi visa 456 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 5,626 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 176,137 kutoka kwa sampuli 1,876,105

Katika visa hivi vipya, 424 ni raia wa Kenya huku 32 wakiwa raia wa kigeni, 266 ni wa kiume na 190 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 92.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 535 wamepona virusi vya corona,439 walipona wakiwa nyumbani huku 96  wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 120,894 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 7 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,428 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 975 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,716 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 100 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).