Kangogo Alifariki kwa Jeraha la Risasi,iliyopitia Ubongo, Fuvu - Upasuaji wa mwili wafichua

Muhtasari
  • Upasuaji wa Caroline Kangogo hatimaye wafanyika
Image: HISANI

Caroline Kangogo alikufa kwa kupigwa risasi na risasi ikipitia kwenye ubongo, fuvu, mtaalam wa magonjwa ya serikali Johansen Oduor amefichua.

Kangogo alijipiga risasi na kufa kwa bastola nyumbani kwa mzazi wake huko Elgeiyo Marakwet mnamo Julai 16, 2021.

Alikuwa amepotea kwa zaidi ya wiki mbili baada ya kudaiwa kuwauwa wanaume wawili.

Oduro alithibitisha kuwa alikufa kwa kujiua baada ya kujipiga risasi kupitia kidevu, na kusababisha uharibifu wa fuvu na ubongo wake.

Daktari wa magonjwa aliongezea kuwa Kangogo alijiua mwenyewe ndani ya bafu nyumbani kwa wazazi wake huko Anin, Elgeyo Marakwet Ijumaa, Julai 16.

Image: Ndanyi Mathews

Poda ya bunduki pia ilipatikana kwenye vidole vyake, na Oduor amesema kwamba kipengee hicho kitachunguzwa zaidi.

Kangogo sasa atazikwa Alhamisi, Julai 29, kulingana na wanafamilia

Mwendazake afisa huyo Caroline anatarajiwa kuzikwa Alhamisi, Julai 29 nyumbani kwa babake kulingana na taarifa kutoka kwa familia.

Uchunguzi wa maiti ulikuwa ufanyika Ijumaa, Julai 23 lakini ulihairishwa kwa sababu Mwanapalojia Oduor hakuwa anapatikana siku hiyo.