DP Ruto agadhabishwa na Kukamatwa kwa Mfanyabiashara Harun Ayadin

Muhtasari
  • DP Ruto agadhabishwa na Kukamatwa kwa Mfanyabiashara Harun Ayadin
Naibu rais William Ruto
Image: Maktaba

Naibu Rais William Ruto Jumamosi Agosti 7 alikashifu serikali kwa kumkamata mfanyabishara Harun Aydin ambaye ni rais kutoka Uturuki.

Naibu Rais William Ruto amesema kuwa mwekezaji wa Uturuki Harun Aydin ni mwathirika wa kiburi cha juu.

Haya yanajiri baada ya Aydin, ambaye alikuwa kwenye msafara katika safari ya Ruto iliyokatizwa Uganda Jumamosi kuzuiliwa na maafisa wa uhamiaji na polisi jijini Nairobi.

Ruto alisema kuwa hii ni janga la uchache wa kisiasa.

"Mwekezaji wa Uturuki, Aydin Harun, ni mwathiriwa wa kiburi cha juu kilichozaliwa na walezi na wafanyabiashara wanaofanya biashara hiyo kuwa jinai

Saa hii hata wawekezaji ambao wako na kibali na wanajulikana na serikali zao tunasema ni magaidi kwa sababu tuko na nia duni za kisiasa. Hii ni kusambaratisha taifa letu la Kenya na mnaturudisha nyuma kwa umaskini mkitafuta nia zenu za kibinafasi Msiba wa uchache wa kisiasa, "Ruto alisema.

Harun Aydin alizuiliwa na maafisa wa uhamiaji wakati alitua Nairobi kutoka Uganda alikokuwa tangu Agosti 2.

Maafisa walisema walitaka kumhoji juu ya hali yake ya uhamiaji, idhini ya kufanya kazi na biashara anayohusika katika mkoa huo.

Ruto alisema Kenya itaharibu sifa yake kwa kuwahusisha wawekezaji na uhalifu wa kigaidia kama vile imemfanyikia Aydin.