(+Picha) Huzuni yatanda Embu wakati wa mazishi ya ndugu 2 waliouwa wakiwa mikononi mwa polisi

Muhtasari
  • Huzuni yatanda Embu wakati wa mazishi ya  ndugu 2 waliouwa wakiwa mikononi mwa polisi 
Image: Hisani

Mazishi ya ndugu wawili, Benson Njiru Ndwiga na Emmanuel Mutura Ndwiga waliouawa wakiwa chini ya ulinzi wa polisi yanaendelea katika kijiji cha Kithagari, Kaunti ya Embu.

Katika picha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, familia ya ndugu hao wawili bado inatafuta haki hata wakati kukamatwa kwa wale waliohusika bado hakujafanywa.

Mama aliyefiwa anaonekana mwenye huzuni,maumivu na machozi alipopokea mwili wa watoto wake.

Maelfu ya Wakenya mitandaoni walijumuika kudai haki kutendeka kufuatia kifo cha ndugu wawili kutoka maeneo ya Kianjokoma, Embu.

Benson Njiru (22) na Emmanuel Mutura (19) ambao walikuwa wanafunzi katika chuo kikuu cha Kabarak na chuo cha mafunzo ya kiteknolojia cha Don Bosco mtawalia wanadaiwa kutoweka baada ya kukamatwa na polisi kutoka kituo cha polisi cha Manyatta mnamo Julai 1.

Baada ya kukamatwa kwao haikujulikana walikokuwa na familia ikaanza juhudi za kuwatafuta.

Swali lililo salia akilini mwa wakenya wengi je haki itatendeka, na waliohusika watatiwa nguvuni?

Hizi hapa baadhi ya picha za hafla ya mazishi yao;

Image: Hisani
Image: Hisani
Image: Hisani
Image: Hisani
Image: HIsani