Ninatengeneza Sh1.5m kwa siku kutokana na kuuza mayai-DP Ruto

Muhtasari
  • Naibu wa Rais William Ruto siku ya Alhamisi aliweka wazi  mali anayomiliki, huku akipinga madai kwamba yeye sio HUstler wa kweli
DP William Ruto
Image: Twitter

Naibu wa Rais William Ruto siku ya Alhamisi aliweka wazi  mali anayomiliki, huku akipinga madai kwamba yeye sio HUstler wa kweli.

Yeye, kwa mara ya kwanza, aliorodhesha hadharani vyanzo vyake vya mapato, akifichua anapata Sh1.5 milioni kwa siku kutoka shamba lake la kuku la Koitalel. Shambani kuna kuku 200,000.

Anamiliki pia hisa 400,000 za kampuni kubwa ya simu ya Safaricom na hisa zaidi 8,000 za Kenya Airways.

"Wacha niwasaidie. Kwa mali 10 walizoorodhesha, karibu asilimia 70 ni yangu na zingine sio zangu ...... kama ile Ekari 15,000 walisema ninamiliki katika ADC, hiyo sio kweli. Wanapaswa kuorodhesha hiyo,

Walisahau kufichua kuwa biashara yangu ya kuku, ambayo waliorodhesha kwenye ekari, ina kuku 200,000 na mtu huyu huuza mayai 150,000 kwa siku, na kufanya Sh1.5 milioni kila siku."Ruto alizungumza.

Baada ya ufichuzi wa serikali juu ya utajiri wake, DP jana alisema "ukaguzi wa maisha" sasa unapaswa kufuata mfano kwa viongozi wengine.

"Wamejaribu kufanya ukaguzi huo wa maisha kwa William Ruto na sio mbaya lakini walipaswa kuendelea kufanya vivyo hivyo kwa watu wengine ili tuweze kumaliza hii. Shida ni nini?

Usemi wake DP ulijiri siu moja baada ya waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i kuorodhesha mali anayomiliki Ruto mbele ya bunge.