Jamaa amuua rafiki yake kwa ajili ya deni la shilingi 20 Meru

Muhtasari
  • Jamaa amuua rafiki yake kwa ajili ya deni la shilingi 20 Meru
Pingu
Image: Radio Jambo

Mwanamume wa miaka 24 yuko mikononi mwa polisi katika kituo ch polisi cha Maua, kwa mauaji ya Kenneth Bundi kwa ajili ya deni la shilingi 20.

Fred Mugambi anadaiwa kumuua Bundi siku ya Ijumaa usiku katika soko la Kambo katika kaunti ya Meru, akimuacha kwa majeraha ambayo yalisababisha kifo chake.

Kwa mujibu wa Usimamizi wa uchunguzi wa makosa ya jinai George Kinoti, mtuhumiwa alikuwa na msaidizi aliyejulikana kama Murangiri Maore, ambaye alikimbia eneo mara baada ya tukio hilo.

"Kwa mujibu wa mashahidi, wawili walikabiliana na marehemu juu ya shilingi 20 aliyokopeshwa  Lakini wakati hakuweza kulipa, walimchapa na kumuacha kama amepoteza fahamu

Alipelekwa katika Hospitali ya Nyambene Level 4na wasamaria wema ambapo alitangazwa amekufa wakati wa kuwasili.

"Wapelelezi wa DCI wa Meru, wamezindua utafutaji  kwa mshirika wa pili katika mauaji.

Hii inakuja miezi minne baada ya mfanyakazi wa migodi  alimpiga na kumuua mwenzake katika eneo la Karai la Naivasha baada ya ugomvi juu ya deni la  Sh50.