Mwanafunzi wa Darasa la 6 aua mwanafunzi mwenzake kwa ajili ya ugali huko Kakamega

Muhtasari
  • Polisi katika Kaunti ya Kakamega wanamshikilia mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 14 anayedaiwa kumuua mwenzake kwa ajili ya Ugali na Kunde

Polisi katika Kaunti ya Kakamega wanamshikilia mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 14 anayedaiwa kumuua mwenzake kwa ajili ya Ugali na Kunde.

Mwanafunzi huyo anaripotiwa kuutupa mwili wa marehemu katika Mto Simakina huko Navakholo, Kaunti ya Kakamega.

OCPD wa Navakholo Richard Omanga alithibitisha kisa hicho akisema, marehemu mwenye umri wa miaka 10 alikuwa akichunga ng'ombe wa familia yake wakati alipovamiwa na kushambuliwa na mwanafunzi mwenzake.

Wanafunzi hao wawili walikuwa majirani.

Inaripotiwa kuwa mwanafunzi huyo wa Darasa la Sita alifika nyumbani kutoka shuleni Alhamisi na akaarifiwa kuwa chakula alichokusudia kula kilikuwa kimeliwa na jirani yake.

Kisha alimfuata na kumpiga kichwani na kifaha butu, na kumuua papo hapo kabla ya kutupa mwili wake mtoni.

Siku ya Ijumaa, mtoto huyo alifika shuleni na kuwaarifu walimu wake kwamba alikuwa amemuua mwenzake 

OCPD pia alisema kwamba kichwa cha marehemu kilikuwa na majeraha ya kichwa, na mwili wake umepelekwa katika makafani ya kuhifadhi maiti ya hopsitali ya rufaa ya Kakamega.