Mahakama ya Eldoret yazuia IEBC kukamilisha usajili wa wapiga kura

Muhtasari
  • Mahakama ya Eldoret yazuia IEBC kukamilisha usajili wa wapiga kura
Image: Mathews Ndanyi

HABARI NA MATHEWS NDANYI;

Mahakama Kuu mjini Eldoret mnamo Jumatatu ilitoa maagizo ya kukataza IEBC kukomesha zoezi lililoimarishwa la usajili wa wapigakura.

Mpiga kura Patrick Cherono aliwasilisha ombi akiteta kuwa IEBC haikuafikia lengo lake la kusajili wapiga kura wapya milioni 4.5.

Usajili ulioimarishwa wa wapigakura ulitarajiwa kukamilika tarehe 2 Novemba.

Mpiga kura huyo aliishtaki IEBC na Bunge, ambalo linafaa kutoa ufadhili kwa tume hiyo.

Jaji Eric Ogolla Jumatatu alisema maagizo yatasalia hadi Novemba 9, kesi itakaposikizwa.

Cherono alienda kortini kupitia wakili Kairia Nabasenge.

Mengi yafuata;