Mwanamume aliyetoroka kutoka mikononi mwa polisi miezi mitano iliyopita akamatwa

Muhtasari
  • Mwanamume aliyetoroka kutoka mikononi mwa polisi miezi mitano iliyopita akamatwa
Pingu
Image: Radio Jambo

Maafisa wa upelelezi wa DCI wamemkamata mkosaji wa kifo, ambaye amekuwa mtoro kwa muda wa miezi mitano iliyopita baada ya kutoroka kutoka mikononi mwa polisi kwa mauaji, ubakaji na wizi wa kutumia nguvu.

Katika taarifa, maafisa hao wa upelelezi walisema kuwa John Muturi Keneya almaarufu Francis Limo Ngugi, alikuwa amezuiliwa na Mahakama Kuu ya Kiambu katika kituo cha polisi cha Karuri mnamo Juni mwaka huu, huku akisubiri kufanyiwa uchunguzi wa kiakili.

"Hata hivyo, mbakaji huyo alikuwa na mipango mingine. Walipokuwa wakipewa mlo wao wa jioni mnamo Juni, 22, mwendo wa saa kumi na mbili na nusu jioni, alijificha kutoka kwa seli kwa njia isiyoeleweka na kutoweka," Kinoti alisema.

Mastaa hao walisema kuwa jambo hilo lilisababisha msako wa mhalifu huyo maarufu, "pia mshukiwa mkuu wa mauaji ya mkewe ambaye alifariki baada ya kuchomwa kisu kifuani, Agosti mwaka jana."

Wapelelezi walipokea taarifa kuhusu mahali aliko mtoro, kupitia njia ya kidokezo ya DCI bila kutaja jina.

"Kikosi kilitumwa mara moja hadi katika mji wa mpakani na baada ya saa chache, mshukiwa alifukuzwa katika maficho yake. Mshukiwa kwa sasa ni mgeni wa serikali," DCI ilisema.