Tumemuomba Mungu aingilie kati-Familia ya Ndugu waliouawa Kianjokoma wanasema wanangoja haki itendeke

Muhtasari
  • Familia ya Ndugu waliouawa Kianjokoma wanasema wanangoja haki itendeke
Mandugu wawili wanaodaiwa kufariki mikononi mwa maafisa wa polisi
Mandugu wawili wanaodaiwa kufariki mikononi mwa maafisa wa polisi
Image: HISANI

Ni takriban miezi 4 tangu ndugu wawili kutoka kianjokoma, kaunti ya KIambu kuaga dunia, lakini maisha kwa wapendwa wao baada ya vifo vyao yamekuwa aje?

Huku familia ya wawili hao ikizungumza na runinga ya Citizen siku ya Jumamosi ilisema kwamba inasubiri haki itendeke, na wala hawajawahi kubaliana na vifo vya wana wao.

“Unajua kama familia tunangojea haki.. kama mzazi…. mmh sijui krismasi itakuwa aje bila wao walikuwa wanatufurahisha,ata sijui ama kuna krismasi, nilipoendea vitu vya NJiru kwenye chuo kikuu nililia sana kwa barabara,” Catherine Wawira, mama wa ndugu  marehemu Kianjakoma alisema.

Baba yao, bado anakumbusha kumbukumbu na nyakati alizounda akiwa na wanawe wawili ambao anawataja kuwa ‘marafiki zangu’.

"Wavulana hawa walilelewa katika imani ya kikatoliki.. Tumemuomba Mungu aingilie kati, kumbukumbu tulizoshiriki, tulishiriki mambo mengi, wavulana hao walikuwa marafiki zangu

Mama yao huwa anatandika vitanda vyao kama njia ya kuungana nao, kwa kweli sijui nini kilichotokea," John Ndwiga, baba wa wawili hao alisema.

Mutura alikuwa ametoka tu kuhitimu kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Wavulana ya Don Bosco na Cheti cha Uhandisi wa Umeme na Jua, huku Njiru akiwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Kabarak.

Familia ya marehemu inasema ilifahamu kuwa miili ya wavulana hao ilipatikana katika kituo cha biashara cha Kibungu, kilomita 10 kutoka walikokamatwa Jumapili usiku.

Baba wa ndugu hao, John Ndwiga, alisema anaamini polisi walihusika na vifo vya watoto wake.

"Nilitazama miili yao na niliweza kusema walipigwa. Nyuso zao zilikuwa zimevimba na walikuwa na michubuko,” alisema.

Wakati huo huo, maafisa sita wa polisi waliofikishwa mahakamani kuhusu mauaji hayo watafikishwa mahakamani tena Januari 25, 2021.

Wale sita; Benson Mbuthia, Consolota Kariuki, Nicholas Cheruiyot, Martin Wanyama, Lilian Cherono na James Mwanikiwere walishtakiwa kwa makosa mawili ya mauaji kila mwezi Septemba.