Ikiwa Raila hatamsaini Kalonzo kwa Azimio, ajitayarishe kutawazwa kwa Ruto-Kuria

Muhtasari
  • Kuria alitoa maoni kwamba athari za kisiasa ambazo Kalonzo angeleta kwa vuguvugu la Azimio la Umoja bado ni kubwa
Mbunge wa Gatunndu Kusini, Moses Kuria
Mbunge wa Gatunndu Kusini, Moses Kuria
Image: MAKTABA

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria sasa anaamini kuwa haiwezekani kwa kiongozi wa ODM Raila Odinga kupata ushindi katika uchaguzi ujao wa urais bila uungwaji mkono wa mkuu wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka.

Kuria alitoa maoni kwamba athari za kisiasa ambazo Kalonzo angeleta kwa vuguvugu la Azimio la Umoja bado ni kubwa kuliko ile iliyoletwa na Magavana wa Ukambani Charity Ngilu (Kitui), Kivutha Kibwana (Makueni) na Alfred Mutua (Machakos) ambao tayari wametangaza kumuunga mkono Odinga.

"Hata Raila anajua hakuna jinsi Charity Ngilu, Alfred Mutua na Kivutha Kibwana wanaweza kuchukua nafasi ya Kalonzo Musyoka," mbunge huyo alisema katika mahojiano na gazeti la Standard.

“Ikiwa Raila hata msaini Kalonzo kwa Azimio, ajitayarishe kutawazwa kwa Ruto, hata kuapishwa.”

Mbunge huyo aliteta kuwa Odinga alifanya makosa makubwa kwa kuwapoteza waliokuwa vinara wawili wa OKA kwa mpinzani wake DP Ruto, ambao ni; Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi na mwenzake wa Ford-Kenya Moses Wetangula.

Alisema licha ya kuingia kwa chama cha Democratic Action Party of Kenya (DAP-K) ambacho kimejaribu kuunganisha kura za eneo la Magharibi za Raila, kupoteza kwa Mudavadi na Wetangula bado kunasalia kuwa pigo kwa siasa za Odinga.

“Kuwapoteza Mudavadi na Wetangula ilikuwa hasara kubwa kwa Raila. Inamaanisha kuwa amefanya kura za Magharibi kuwa mojawapo ya maeneo anayopaswa kufanya kazi fulani ilhali inaweza kuwa matembezi,” alisema Kuria.

"Kwa upande mzuri zaidi, Eugene Wamalwa na kikosi chake cha DAP wamechukua hatua haraka ili kupunguza uharibifu kwa Baba lakini kupoteza wawili hao kuliepukika."

Aidha mbunge huyo alidai kuwa alipokea mwaliko wa nafasi ya naibu rais kutoka katika kambi mbili kuu za kisiasa lakini alidai kuwa amezikataa ili kuelekeza nguvu zake katika kujenga chama chake cha Chama Cha Kazi (CCK).