Moses Kuria atangaza azma ya kuwania ugavana wa Kiambu

Muhtasari

•Mbunge huyo wa muhula wa pili ameashiria kuwa atawania kiti hicho kutumia tikiti yachama chake cha  'Chama Cha Kazi' 

•Bango ambalo Kuria alipakia lilkuwa na maandishi "Moses Kuria. Gavana wa Kiambu 2022. Heri upande wa Mungu"

Mbunge wa Gatunndu Kusini, Moses Kuria
Mbunge wa Gatunndu Kusini, Moses Kuria
Image: MAKTABA

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amedokeza atakuwa kwenye kinyang'anyiro cha ugavana wa Kiambu katika uchaguzi wa mwezi Agosti.

Kupitia chapisho la Facebook,mbunge huyo wa muhula wa pili ameashiria kuwa atawania kiti hicho kutumia tikiti ya Chama Cha Kazi (CCM)  ambacho anaongoza.

Kuria ambaye alirejea nchini wiki moja iliyopita baada ya kulazwa katika hospitali ya Dubai kwa miezi mitatu analenga kuwa gavana wa nne wa kaunti hiyo yenye wapiga kura zaidi ya milioni moja.

"Sauti ya watu ni sauti ya Mungu. Nisaidie Mungu. Chini ya mabawa yako najisikia salama," Kuria aliandika chini ya picha ya bango la kampeni ambayo alipakia.

Bango ambalo Kuria alipakia lilkuwa na maandishi "Moses Kuria. Gavana wa Kiambu 2022. Heri upande wa Mungu"

Kuria atamenyana na wanasiasa wengine wakiwemo gavana wa sasa James Nyoro, Seneta Kimani Wamatangi, gavana wa zamani William Kabogo, Mbunge wa Thika Patrick Wainaina, spika wa bunge la 

ambao wameonyesha nia ni Nyoro, seneta wa Kiambu Kimani Wamatangi, Mbunge wa Thika Mjini Patrick Wainaina, mhadhiri wa Chuo Kikuu Juliet Kimemia, Spika wa Bunge la Kaunti ya Kiambu Stephen Ndichu miongoni mwa wengine.