Ruto atimuliwa kama naibu kiongozi wa Jubilee

Muhtasari

•Rais Uhuru Kenyatta amechaguliwa kuwa kiongozi wa Jubilee Party kwa muhula mwingine wa miaka mitano.

Rais Uhuru Kenyatta na naibu rais William Ruto
Rais Uhuru Kenyatta na naibu rais William Ruto
Image: HISANI

Naibu Rais William Ruto ametimuliwa kama naibu kiongozi wa chama tawala cha Jubilee.

Wakati huo huo rais Uhuru Kenyatta amechaguliwa kuwa kiongozi wa Jubilee Party kwa muhula mwingine wa miaka mitano.

Hii ina maana kuwa rais atashiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa Agosti 2022.

Viongozi wengine wapya wa kitaifa ambao wameteuliwa akiwemo Mbunge wa Ndaragwa Jeremiah Kioni ambaye atachukua nafasi ya katibu mkuu Raphael Tuju.

David Murathe amesalia kama naibu mwenyekiti wa chama hicho chini ya Nelson Nzuya.

Mbunge wa Kitutu chache kaskazini Jimmy Angwenyi ni mmoja wa manaibu viongozi wanne wa chama cha Jubilee.

Wengine walioteuliwa  ni Katobu Ngatobu, Naomi Shaban na Peter Mositet.

Mbunge wa Kieni Kanini Kega ameteuliwa kama mkurugenzi wa uchaguzi wa chama cha Jubilee.