Raphael Tuju ajiuzulu kama katibu mkuu wa Jubilee

Muhtasari

•Tuju amesema anamshukuru rais kwa kumkabidhi na wadhifa huo licha yake kutoka karibu na nyumbani kwa mpinzani wake mkuu.

•Rais Kenyatta amesihi kinara wa ODM Raila Odinga ambaye ndiye mridhi wake wa chaguo lake amuunge Tuju mkono katika siku zijazo

Katibu mkuu wa Jubilee
Katibu mkuu wa Jubilee
Image: MAKTABA

Raphael Tuju amejiuzulu kama katibu mkuu wa Jubilee.

Mbunge huyo wa zamani wa Rarienda amesema anamshukuru rais kwa kumkabidhi na wadhifa huo licha yake kutoka karibu na nyumbani kwa mpinzani wake mkuu.

“Asante kwa kusimama nami hata katika ngazi ya kibinafsi nilipopata ajali mbaya mpaka sasa hivi naweza kusimama hapa" Tuju alisema.

Tuju hakufichua mpango wake baada ya kujiuzulu lakini alisema rais amempa majukumu mengine katika siku zijazo.

"Tumekubaliana na rais kwamba atanipa majukumu mengine kwenda mbele," Tuju alisema.

Aliendelea:"Siwezi kuwa katibu mkuu na pia kutafuta malengo mengine ya kisiasa na kazi zingine alizonipa.'

Chama hicho leo kinatarajiwa kutangaza mabadiliko makubwa zaidi katika chama huku kikijipanga upya kwa utayari wa kujiunga na Azimio La Umoja.

 Rais Kenyatta amesihi kinara wa ODM Raila Odinga ambaye ndiye mridhi wake wa chaguo lake kumuunga Tuju mkono katika siku zijazo.