Wawili wafariki baada ya choo kuporomoka Ongata Rongai

Muhtasari

•Wafanyakazi hao wawili walikuwa wakirekebisha upande wa ukuta wa choo hicho uliokuwa umepasuka.

•Maafisa wa kaunti walitembelea eneo la tukio na kuamuru choo hicho kujazwa na wapangaji wapatao 10 kuhamishwa hadi sehemu  nyingine.

Watu watatu waliokolewa baada ya shimo la choo cha futi 20 kuporomoka din Kwale.
Watu watatu waliokolewa baada ya shimo la choo cha futi 20 kuporomoka din Kwale.
Image: SHABAN OMAR

Wanaume wawili waliokuwa wakitengeneza choo cha shimo katika mtaa wa Ongata Rongai, kaunti ya Kajiado walipoteza uhai wao kilipoporomoka.

Wafanyakazi hao wawili walikuwa wakirekebisha upande wa ukuta wa choo hicho uliokuwa umepasuka siku ya Jumatatu.

Polisi na maafisa wa zimamoto waliitwa kwenye eneo la tukio ili kuchukua miili kutoka mahali ilipokuwa imekwama.

Miili hiyo ilipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kwa uchunguzi.

Maafisa kutoka kaunti ya Kajiado walitembelea eneo la tukio na kuamuru choo hicho kujazwa na wapangaji wapatao 10 kuhamishwa hadi sehemu  nyingine hadi wakati choo kipya  kiitakapojengwa.

Wakati huo huo, polisi wanachunguza kisa ambapo mwanamume mmoja alidungwa kisu na kujeruhiwa vibaya na watu wengine wawili wanaoaminika kuwa wanachama wa kikundi maalum katika vita vilivyotokea katika chumba cha wageni jijini Nairobi.

Polisi wanasema wanaume wawili walilipia  chumba kwanza Lodging  hiyo kabla ya mtu wa tatu  kuungana nao.

Mwanaume wa tatu alimwambia mhudumu wa nyumba hiyo kwamba alikuwa akijiunga na marafiki zake kwa mkutano katika chumba namba 33.

Baadae vita vilizuka.  Wawili wao walimdunga mwenzao kwenye kiwiliwili mara nne na kutoroka. Sababu hazikutambuliwa mara moja.

Mhudumu katika hoteli hiyo  iliyo karibu na River Road aliwaambia polisi kwamba alisikia zogo kutoka chumbani na kwenda kuangalia, na kuwapata wanaume hao wakikimbia. Mmoja wao alikuwa akivuja damu.

Mmoja wa watu hao alikamatwa baadaye walipokuwa wakijaribu kutoroka na kuwaambia polisi kuwa walitofautiana wakielekea hotelini pale, jambo ambalo lilisababisha vita hivyo.

Mhasiriwa ambaye  alijeruhiwa alipelekwa hospitali, akatibiwa  na kuruhusiwa kuenda nyumbani.

Mshukiwa anatarajiwa kukabiliwa na mashtaka mbalimbali ya kushambulia na kusababisha madhara mwilini.

Polisi walisema wanamsaka mshukiwa wa pili ili kufahamu sababu za mapigano hayo.