Mvutano kati ya wanafunzi kuhusu imani za kidini-Shule ya Upili ya Dagorreti

Muhtasari

•Bodi ya usimamizi imeitwa shuleni kwa majadiliano kuhusu jinsi maswala haya yanaweza tatuliwa.

•Bastola ya Jericho ilikuwa imeibiwa kutoka kwa afisa wa polisi huko Parklands, Nairobi mnamo 2019.

Nembo ya Shule ya Upili ya Dagoretti
Nembo ya Shule ya Upili ya Dagoretti
Image: MPASHO.CO.KE

Polisi wametumwa katika shule ya upili ya Dagorreti jijini Nairobi kufuatia mvutano kati ya wanafunzi kuhusu imani za kidini.

Polisi wanasema mvutano huo ulianza Jumapili jioni baada ya mchuano wa soka  hadi usiku kucha na kusababisha hatua za polisi kuingia humo.

Bodi ya usimamizi imeitwa shuleni kwa majadiliano kuhusu jinsi maswala haya yanaweza tatuliwa.

Kwingineko ni kwamba,Bastola ambayo ilipatikana kutoka kwa washukiwa watatu waliouawa imethibitishwa kuwa ya polisi.

Bastola ya Jericho ilikuwa imeibiwa kutoka kwa afisa wa polisi huko Parklands, Nairobi mnamo 2019.

Silaha hiyo ilipatikana kutoka kwa washukiwa watatu waliokuwa wamevamiwa na kundi la watu baada ya kumwibia mhudumu wa Mpesa eneo la Marurui, kando ya barabara ya Kaskazini.

Washukiwa hao walikuwa wamemwibia mhudumu huyo na kujaribu kutoroka wakati ambayo tahadhari ilipotangazwa kuwatahadharisha wananchi.

Wakati huo huo, Kikosi maalum kimetumwa mjini Nakuru kufuatilia genge lililo shiriki katika  msururu wa mashambulizi ambayo yameshuhudiwa katika eneo hilo.

Hadi sasa washukiwa 27 wametiwa mbaroni kuhusiana na visa vya ujambazi wa kutumia silaha ambavyo vimeripotiwa mjini humo katika siku chache zilizopita.

Washukiwa wengine walikamatwa katika operesheni tofauti iliyoendeshwa ni wenye umri wa kati ya miaka 20 na 30.

Wapelelezi wanaonya majambazi waliosalia kujisalimisha.