(+PICHA)Mtu 1 aaga dunia Kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya barabara ya Nairobi Expressway

Muhtasari
  • Mtu 1 aaga dunia Kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya barabara ya Nairobi Expressway
Image: EZEKIEL AMING'A

Mtu mmoja alifariki na idadi isiyojulikana kujeruhiwa baada ya ajali kutokea kwenye barabara kuu ya Nairobi Jumamosi usiku. Ajali ya saa 10 Jioni iliyotokea katika kituo cha Mlolongo ilihusisha magari kadhaa.

Kulingana na Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu ya Kenya, dereva aliyekuwa akitoka kwenye kituo cha utozaji ushuru alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi na kugonga Toll booth na magari mengine.

Mtu 1 aaga dunia Kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya barabara ya Nairobi Expressway
Image: GRACE MUIA

"Mwendesha gari aligonga kwenye Toll Plaza na kuyapita magari mengine ambayo yalikuwa yanaruhusiwa kutoka. Kwa hivyo gari liligonga kituo kimoja cha ushuru na kumjeruhi mhudumu mmoja kando ya madereva wengine,” mamlaka ilisema katika taarifa Jumapili asubuhi.

Watu waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali za karibu, na inasemekana wanaendelea vyema na matibabu.

Image: GRACE MUIA

Hata hivyo, KENHA imetangaza kufunga njia ya kutoka katika kituo cha Ushuru cha Mlolongo, na kuwahakikishia madereva kwamba wataweka mikakati ya kuepusha matukio hayo.

 

Wenye magari wanashauriwa zaidi kuepuka mwendo kasi kwenye miundombinu iliyojengwa hivi karibuni.