Mauaji ya Zawahiri ‘yatahitimisha kipindi cha majonzi’ kwa waathiriwa wa Kenya

Mashambulio ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania ni mojawapo ya mashambulizi ya awali ya al-Qaeda.

Muhtasari

•Mauaji ya Ayman al-Zawahiri ‘yatahitimisha kipindi cha majonzi’ kwa wahasiriwa wa Kenya waliojeruhiwa katika shambulio la al-Qaeda kwenye ubalozi wa Marekani, Nairobi.

•Douglas Sidialo, msemaji wa chama cha wahasiriwa wa Kenya, alitaja mauaji ya al-Zawahiri kama ‘’tendo la Mungu’’.

alipoteza uwezo wake wa kuona katika shambulio la ubalozi wa Marekani mjini Nairobi mwaka wa 1998
Douglas Sidialo (kushoto) alipoteza uwezo wake wa kuona katika shambulio la ubalozi wa Marekani mjini Nairobi mwaka wa 1998
Image: BBC

Mauaji ya Ayman al-Zawahiri ‘yatahitimisha kipindi cha majonzi’ kwa wahasiriwa wa Kenya waliojeruhiwa katika shambulio la al-Qaeda kwenye ubalozi wa Marekani huko Nairobi miaka 24 iliyopita.

Mashambulio hayo mawili dhidi ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania ni mojawapo ya mashambulizi ya awali ya al-Qaeda na yalisababisha vifo vya zaidi ya 200 siku hiyo hiyo.

Douglas Sidialo, msemaji wa chama cha wahasiriwa wa Kenya, alitaja mauaji ya al-Zawahiri kama ‘’tendo la Mungu’’.

Aliambia kipindi cha Newsday cha BBC: ‘’Ni vizuri imetokea - kwamba wanawajibisha wale waliohusika na vitendo hivi viovu na vya kinyama.’’

Lakini alilalamika kuwa hasara kwa familia za Kenya za wahasiriwa au wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo hazijalipwa.

Haya yanajiri licha ya ahadi ya Joe Biden mnamo mwaka 2010, alipokuwa makamu wa rais, ya kuangazia swala la fidia alipozuru Nairobi.

‘’Najua raia wa Marekani, wanakandarasi na wafanyakazi wa ubalozi huo walilipwa... lakini sisi kama Wakenya hatujawahi kuzingatiwa katika kulipwa fidia.’’

Na hii imekuwa maumivu.

‘’Najua raia wa Marekani, wanakandarasi na wafanyakazi wa ubalozi huo walilipwa fidia... lakini sisi kama Wakenya hatujawahi kufikiriwa kulipwa fidia.Na hii imekuwa maumivu.’’

‘’ Wamarekani wanapaswa kujitokeza na kuhakikisha kwamba sisi waathiriwa wa Kenya tunalipwa’’.

Lazima tuhakikishe haki za binadamu za Wakenya zinashughulikiwa sawa na Wamarekani.

‘’Wamarekani wanapaswa kujitokeza na kuhakikisha kwamba sisi wahasiriwa wa Kenya tunalipwa. Lazima tuhakikishe haki za binadamu za Wakenya zinashughulikiwa sawa na Wamarekani.’’