Aliyekuwa mtangazaji wa KBC Laban Karani afariki

Karani ameacha mke na watoto wawili.

Muhtasari

• Kifo cha Karani kiliwekwa hadharani na mkewe Rhoda Karani huku kukiwa na ufichuzi kuwa Mtangazaji huyo wa zamani wa TV alifariki Juja Nyumbani kwao.

• Marehemu Mwandishi huyo wa Habari alikuwa akipambana na ugonjwa wa kisukari na Presha.

Aliyekuwa mtangazaji wa KBC Laban Karani amefariki
Aliyekuwa mtangazaji wa KBC Laban Karani amefariki

Wanahabari nchini Kenya wanaomboleza kifo cha ghafla cha mwanahabari nguli Laban Karani.

Kifo cha Karani kiliwekwa hadharani na mkewe Rhoda Karani  huku kukiwa na ufichuzi kuwa mtangazaji huyo wa zamani wa alifariki nyumbani kwao Juja.

Marehemu mwanahabari alikuwa akipambana na ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu mwilini. 

"Ni wakati wa kusikitisha sana kwa familia.

Alikuwa akitibiwa ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu, na hali yake ilizidi kuwa ngumu. Katika miezi michache iliyopita, alikuwa akiingia na kutoka hospitalini hadi alipougua ugonjwa huo," Rhoda Karani alibainisha.

Karani ameacha mke na watoto wawili.

Mtangazaji mkongwe Obachi Mochoka ni miongoni mwa Wakenya ambao wameomboleza kifo cha mwanahabari huyo mkongwe.

"Siku zote alikuwa mtu mwenye furaha, na alikumbatia sisi katika tasnia, tayari kufanya kazi nasi," Machoka aliandika.

Laban Karani alikuwa mwanahabari kwa zaidi ya miaka 22 - kwa muda mwingi wa miaka yake katika KBC.

Alijiunga na Shirika la Utangazaji la Kenya mnamo 1990 baada ya kuhitimu kutoka Taasisi ya Mawasiliano ya Kenya  (KIMC), ambapo alifanya kazi kama mhariri kwenye dawati la redio na TV.

Katika KBC, Karani aliwasilisha habari za Kiswahili na kuandaa kipindi cha 'Dunia Wiki hii.' Mnamo 1998, alihamia MediaMax hadi 2012 alipoacha kujiunga na siasa.

Baadaye alichaguliwa kuwa mwanachama wa bunge la Kaunti ya wadi ya Mwimbi katika Kaunti ya Tharaka Nithi.