JSC yamteua Jaji Ouko kuwa jaji wa Mahakama ya juu

Muhtasari
  • JSC yamteua Jaji Ouko kuwa jaji wa Mahakama ya juu
Jaji William Ouko
Image: Fredrick Omondi

Jaji wa Rufaa William Ouko ameteuliwa kuwa jaji wa Mahakama ya juu.

Tume ya Huduma ya Mahakama Jumatano ilikubaliana kwa kauli moja juu ya uteuzi wake.

Atajiunga na korti kuchukua nafasi ya Jaji Jackton Ojwang aliyestaafu mnamo Februari mwaka jana.

JSC ilikuwa imeorodhesha wagombea wote tisa walioomba nafasi hiyo. Wale walioomba kujiunga na korti kuu ni pamoja na Jaji Ouko na wenzake wa Mahakama ya Rufaa Koome, Kathurima M'Inoti, Majaji wa Mahakama Kuu Joseph Sergon na Chitembwe, Prof Lumumba Nyaberi, Bi Yano na Majaji Marete na Nderi.

Mengi yafuata;