Makamishna 4 wa IEBC wakula kiapo cha ofisi

Muhtasari
  • Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati Alhamisi aliwakaribisha makamishna 4 katika IEBC saa chache baada ya kula kiapo
Image: IEBC/Twitter

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati Alhamisi aliwakaribisha makamishna 4 katika IEBC saa chache baada ya kula kiapo.

Juliana Cherera, Francis Mathenge, Irene Masit, na Justus ABonyo. Wanatarajiwa kutumikia kwa miaka sita.

Rais Uhuru Kenyatta alichapisha ujumbe wa kuwateua makamishana hao siku ya Alhamisi.

Nafasi hizo ziliachwa wazi baada ya kuondoka kwa Roselyne Akombe, Paul Kurgat, Connie Maina, na Margaret Mwachanya baada ya uchaguzi mkuu wa 2017.

Mapema siku ya Alhamisi Mahakama Kuu ilikataa kutoa maagizo ya kuzuia kuapishwa kwa Makamishna wanne wa IEBC walioteuliwa hivi karibuni.

Jaji Weldon Korir, katika uamuzi mfupi Alhamisi, alibainisha kuwa nchi inaelekea kwenye uchaguzi na kucheleweshwa zaidi kwa kuapishwa kwa makamishna kuna hatari kwa Wakenya.

"Ni kwa maslahi ya umma kwamba amri za kihafidhina hazipaswi kutolewa" korti iliamua.