Raila Odinga aomba msamaha kwa matamshi yake ya madoadoa

Muhtasari

• Kiongozi wa ODM Raila Odinga ameomba msamaha kuhusu matamshi yake ya ‘madoadoa’ aliyoyatoa katika kaunti ya Wajir.

• “…Naomba niseme pole kawa yale maneno niliongea huko Wajir, nilimaanisha watu wote wa Wajir wako Azimio,” Odinga alisema.

Image: TWITTER// RAILA ODINGA

Kiongozi wa ODM Raila Odinga ameomba msamaha kuhusu matamshi yake ya ‘madoadoa’ aliyoyatoa katika kaunti ya Wajir.

Akizungumza katika kaunti ya Kisumu Ijumaa, Odinga alisema pole kwa wote ambao walikwazika kwa matamshi yake.

“…Naomba niseme pole kawa yale maneno niliongea huko Wajir, nilimaanisha watu wote wa Wajir wako Azimio,” Odinga alisema.

Odinga alizungumza haya baada kuagizwa kufika katika tume ya NCIC ili kujibu mashtaka kuhusu matamshi ya kuchochea chuki aliyoyataja huko Wajir.

Raila alishikilia kwamba vuguvugu la Azimio linazidi kupata umaarufu kote nchini huku viongozi zaidi wakizidi kujiunga na kambi hiyo.

Ikumbukwe kwamba seneta wa Meru Mithika Linturi alikamatwa wiki chache zilizopita kwa kutumia neno madoadoa kwenye kampeni za chama cha UDA katika eneo la bonde la ufa.