Historia ya rais wa tatu wa Kenya, hayati mzee Mwai Kibaki

Muhtasari

• Mwai Kibaki alikuwa rais wa tatu wa Jamhuri ya Kenya kuanzia 2002 hadi 2013 akiwa ametanguliwa na Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta na rais wa pili Daniel Arap Moi. Jina lake la kubatizwa ni Emilio Stanley .

Mzee Mwai Kibaki alizaliwa mnamo tarehe 15/11/ 1931, katika kijiji cha Gatuyaini,tarafa ya Othaya, kaunti  ya Nyeri.

Mwai Kibaki alikuwarais   wa tatu wa jamhuri ya Kenya  kuanzia 2002 hadi 2013 akiwa ametanguliwa na rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta na rais wa pili Daniel Arap Moi.  Jina lake la kubatizwa ni Emilio Stanley .

Kibaki alisoma uchumi, historia na sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda.

Akiwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere, Kibaki alikuwa ni mwenyekiti wa chama cha wanafunzi toka Kenya , Kenya Students' Association. Alipomaliza masomo yake mwaka 1955 alipewa tuzo kutokana na kufanya vyema katika mitihani.

Tuzo hiyo ilimwezesha kwenda kusoma katika chuo cha London School of Economics. Alipomaliza masomo alikwenda kufundisha katika chuo kikuu cha Makerere. Baadaye aliacha kazi ya kufundisha na kuwa mtendaji mkuu wa chama cha Kenya African Naytional Union.

Kibaki, licha ya kuwa mbunge, amewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwenyekiti wa Tume ya Mipango, Waziri wa Biashara na Viwanda, na Waziri wa Fedha. Moi alipoingia madarakani baada ya kifo cha Jomo Kenyatta, Kibaki aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais.

Mwaka 1988 Kibaki alianza kuwa na mgongano na Rais Moi. Mwaka huo alivuliwa Umakamu wa Rais na kupelekwa Wizara ya Afya.

Mwaka 1991 Kibaki aliondoka chama cha KANU na kuanzisha chama cha Democratic Party. Katika uchaguzi wa Urais wa mwaka 1991, Kibaki alikuwa wa tatu na mwaka 1997 alikuwa wa pili.

Uchaguzi wa 28 Desemba 2007 ulimrudisha Kibaki kwa kipindi cha pili kama rais. Uchaguzi huu ulipingwa na chama cha upinzani,ODM , na watazamaji wa kimataifa kuwa matokeo hayo hayakuwakilisha matakwa ya Wakenya. Mpinzani wake mkuu, Raila Odinga  alikuwa mbele katika hesabu za kura hadi Kamati ya Uchaguzi iliposimamisha kuhesabu; baada ya kuendelea na matanganzo Kibaki alionekana kuwa mbele.

Mungu ailaze roho yake mahali npema penye wema.