Mjukuu wa Kibaki: Nimenyoa rasta, sikupenda vile zinahusishwa na mambo fulani

Muhtasari

• Sean Andrew aliamua kunyoa rasta kwa kuchukizwa na jinsi zilivyokuwa zikihusishwa na mambo fulani.

Sean Andr3w
Image: Instagram

Mjukuu wa rais wa tatu wa Kenya Mwai Kibaki Jumatano aliwashangaza wengi baada ya kupakia video kwenye Instagrma yake akiwa kwenye kinyozi huku akikatwa nywele zake ndevu, maarufu kama ‘rastas’ ambazo wengi wamekuwa wakizijua kama nembo ya utambulisho wake.

Sean Andrew ambaye ni mfanyibiashara na mkuza maudhui mtandaoni Instagram aliahidi wafuasi wake kwamba angetoa sababu za kufikia uamuzi wa kukata rasta zake ambazo amezilea kwa Zaidi ya miaka mitano.

Na kweli na ahadi zake, Andrew hakuwafeli wafuasi wake waliokuwa ange kusubiri sababu zake za kutafuta muonekano mpya. Katika video ambayo aliipakia usiku wa Jumatano kwenye ukurasa wake wa Instagram, Andrew ameelezea sababu haswa za kuzikata rasta zake.

Amesema kwamba alifikia hatua hiyo baada ya tathmini ya muda mrefu na yote ni kwa sababu hakupenda jinsi ambavyo watu walikuwa wanahusisha rasta na mambo mengine, mawazo fulani ambayo hayakumfurahisha vile na hivyo kuamua kutafuta muonekano wa kawaida ambao utamfanya kuacha kufikirika vibaya.

“Najua mnashangaa sana mbona nikabilisha kutoka kulea rasta, hadi kuzinyoa. Mimi sikuwa najali kufuga rasta, ila tu ni meamua kuzikata kwa sababu sikupenda jinsi ambavyo zilikuwa zinahusishwa na masuala fulani, unajua, mawazo, dhana na mambo mengine mengi. Kama ilivyo kwa hivi sasa, maisha yangu yako mbali sana na kule nilikotegemea yatakuwa, na ni heri nijulikana kutokana kwa vitendo vyangu, vibaya au vizuri kuliko kujulikana na nywele zangu au hata mahusiano yangu na vitu au watu,” anasikika akisema kwenye video hiyo.

Je, unahisi ni mambo au vitu vipi hivi ambavyo Sean Andrew alihusishwa navyo vikamchukiza mpaka kupelekea yeye kukata rastas?