Sakaja amchagua bosi wa Absa James Muchiri kama mgombea mwenza wake

Muhtasari
  • Sakaja alifichua kuwa aliangalia nguzo tano wakati akimchagua mgombea mwenza wake
Johnson Sakaja
Johnson Sakaja
Image: Ezekiel Aming'a, KWA HISANI

Mgombea ugavana wa Nairobi Johnson Sakaja amemtaja Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Absa Bank Kenya Ltd James Njoroge Muchiri kuwa mgombea mwenza wake.

Akizungumza na gazetti la Star, Sakaja alifichua kuwa aliangalia nguzo tano wakati akimchagua mgombea mwenza wake, ikiwa ni pamoja na nguvu na ukakamavu na umakini wa kibiashara.

"DG alipaswa kuwa na moyo wa watu. Mtu ambaye anaweza kujihusisha kwa urahisi na maisha ya wakazi wa Nairobi na anayeweza kuhusika na mahitaji yao ya kila siku. Mtu ambaye hatakuwa na shida kuungana na watu," alisema.

Timu ya Sakaja-Muchiri itakabiliana na wawili hao wa Azimio - mtendaji mkuu wa shirika Polycarp Igathe na aliyekuwa Mbunge wa Kibwezi Prof Philip Kaloki ambao watakuwa wakipeperusha bendera ya Azimio jijini Nairobi.

Haya yanajiri saa chache baada ya IEBC, kuongeza muda wa kuwasilisha wagombea wenza wa urais na ugavana.