Rais Ruto achapisha majina ya mawaziri kwenye gazeti la serikali

Zacharia Njeru (Makazi), Susan Wafula (Afya), Mithika Linturi (Kilimo), Eliud Owalo (ICT) na Ezekiel Machogu (Elimu).

Muhtasari
  • Katika notisi ya gazeti la serikali iliyotolewa Jumatano, Ruto pia alimteua Mercy Wanjau kuwa Katibu wa Baraza la Mawaziri

Rais William Ruto ametangaza kwenye gazeti rasmi la serikali mawaziri 22 waliopendekeza na kisha kuidhinishwa  na bunge la kitaifa.

Katika notisi ya gazeti la serikali iliyotolewa Jumatano, Ruto pia alimteua Mercy Wanjau kuwa Katibu wa Baraza la Mawaziri.

“Katika kutekeleza mamlaka yaliyotolewa na Ibara ya 156 (2) ya Katiba, mimi, William Samoei Ruto, Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, namteua Justin Muturi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuanzia Oktoba 27," ilani hiyo iliongeza.

Mawaziri hao ni pamoja na Aden Duale (Ulinzi), Alfred Mutua (Masuala ya Kigeni), Alice Wahome (Maji), Kithure Kindiki (Ndani) na Njuguna Ndung'u (Hazina) .

Davis Chirchir (Nishati), Moses Kuria (Biashara), Kipchumba Murkomen (Uchukuzi), Soipan Tuya (Mazingira) na Peninah Malonza (Utalii).

Zacharia Njeru (Makazi), Susan Wafula (Afya), Mithika Linturi (Kilimo), Eliud Owalo (ICT) na Ezekiel Machogu (Elimu).

Wengine ni Ababu Namwamba (Michezo), Rebecca Miano (EAC), Simon Chelugui (Ushirika), Salim Mvurya (madini), Aisha Jumwa (Jinsia) na Florence Chepngetich (Kazi).