RIP! Mamake wakili Donald Kipkorir aaga dunia baada ya vita ya muda mrefu dhidi ya saratani

"Mama yangu kipenzi, Katarina alipumzika na yuko kifuani mwa Abraham," alisema.

Muhtasari

• "Mama yangu kipenzi, Katarina alipumzika na yuko kifuani mwa Abraham," alisema.

 
• Kipkorir alisema mamake alipambana na saratani yake kali kwa "ustahiki, uaminifu kwa Mungu na ujasiri".

Katarina, mamake Donald Kipkorir ameaga dunia kutokana na saratani.
Katarina, mamake Donald Kipkorir ameaga dunia kutokana na saratani.
Image: STAR

Wakili Donald Kipkorir yuko katika majonzi baada ya mamake kuaga dunia alipokuwa akipatiwa matibabu ya saratani nchini India.

Mama yake, Katarina alifariki Jumamosi.

"Mama yangu kipenzi, Katarina alipumzika na yuko kifuani mwa Abraham," alisema.

Kipkorir alisema mamake alipambana na saratani yake kali kwa "ustahiki, uaminifu kwa Mungu na ujasiri".

"Hakuwahi kulia hata mara moja katika maumivu yake ya kuungua. Namshukuru Mungu kwa kunipa. Akiwa mbinguni, anapata amani na utulivu," alisema.

"Saluti kwa Mama huzuni bila maumivu, utupu, giza,”

Mama yake alisafirishwa hadi India mnamo Mei 19.

Kisha Kipkorir alisema mama huyo alipaswa kuonana na daktari wa saratani.

"Nikiwa njiani kuelekea India na mama yangu. Mama yangu Kipenzi Katarina amepata maumivu makali sana. Nikiwaombea wataalam bora wa magonjwa ya saratani nchini India wampe mama yangu ahueni na uponyaji. Mbingu zitusikie," alisema.

Mamake Kipkorir amekuwa akiugua kwa muda mrefu.

Mama yake, Katarina alifariki Jumamosi.

"Mama yangu kipenzi, Katarina alipumzika na yuko kifuani mwa Abraham," alisema.

Alikuwa akifanyiwa matibabu ya radiotherapy hapa nchini Kenya kabla ya kusafirishwa hadi India.